Jeshi la Polisi nchini Kenya linamshikilia Mwanaume wa miaka 30 kwa tuhuma za kumlazimisha Mtoto wa miaka 2 kunywa bia wakati wa Siku Kuu ya Krismasi

Baada ya tukio hilo, Wanafamilia walimkimbiza Mtoto huyo Hospitali wakihofia kuwa Mtoto huyo anaweza kupoteza maisha

Wanakijiji waliandamana hadi Kituo cha Polisi kutoa taarifa ya tukio hilo na kusaidia kukamatwa kwa Mercus Kinyua ambaye anatuhumiwa kwa kumnywesha bia Mtoto huyo

Polisi wameonya tabia hiyo na kuongeza kuwa hali ya Mtoto ilikuwa mbaya kwani tayari kiywaji hicho kilimlevya