Jeshi la Polisi Mkoa wa Kusini Unguja linamshikilia Mussa Dude Mussa kwa tuhuma za kumshambulia kwa mabapa ya panga  Doto Dalali Mshanga huko dunga Wilaya Kati.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo la kushambuliwa kimwili Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Unguja Kamishna Msaidizi Suleiman Hassan Suleiman amesema tukio hilo lilitokea mnamo tarehe 9-03-2020 majira ya saa 1:30 usiku huko Messi ya JWTZ Dunga .

Ameongeza kusema kuwa Mussa Dude Mussa mwenye umri wa miaka 26 Mkaazi wa Kidimni ambae alimshambulia Doto Dalali Mshanga mwenye umri wa miaka 30 Mkaazi wa Machui na kumsababishia  maumivu makali katika mwili wake ambapo hadi taarifa hii inatumwa mtuhumiwa wa tukio hilo yupo chini ya ulinzi kwa hatua za kisheria

Rauhiya Mussa