Mbunge mmoja wa Bunge la Senate kutoka jimbo la Queensland nchini Australia, Larissa Waters, ameweka historia bungeni hapo baada ya kwenda na mtoto wake wa miezi miwili na kumnyonyesha bungeni humo jambo ambalo lilitengeneza  historia  nchini humo.

 

Larissa Waters amerejea kazini baada ya likizo ya uzazi na mwanaye huyo, huku akiwa tayari kutumia uhuru wake wa sheria mpya inayowaruhusu wazazi ambao ni maseneta nchini Australia kuja na vichanga vyao na vilevile kuwanyonyesha punde wanapopatwa na njaa.