Mbunge wa Geita Joseph Musukuma leo amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Geita, kujibu tuhuma zake zinazomkabili, baada ya kushikiliwa na polisi tangu Jumapili ya wiki iliyopita.

Akizungumza na mwandishi wa habari wa kituo cha Tv, Kamanda wa Polisi mkoa wa Geita Mponjoli Mwabulambo, amethibitisha kumpeleka Mahakamani mbunge huyo, ambaye anatuhumiwa kuhusika na kuratibu vurugu katika mgodi wa GGM mkoani humo.“Wamepelekwa Mahakamani asubuhi hii”, amesikika Kamanda Mwabulambo akisema

Mbunge Joseph Musukuma pamoja na baadhi ya madiwani na wananchi, walikamatwa na polisi kwa kufunga njia inayoeleka kwenye mgodi wa GGM na kuleta vurugu, kushinikiza mgodi huo kulipa dola