Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimethibitisha Mbunge wake wa viti maalum kutokea Zanzibar, Zainab Mussa Bakari kupata ajali katika eneo la Dumila mkoani Morogoro alipokuwa akitokea Jijini Dodoma kuja Dar es salaam kufuatia kuahirishwa kwa vikao vya Bunge.

Ndugu Zainab amepata ajali ya gari eneo la Dumila mkoani Morogoro wakati akitoka jijini Dodoma kwenda Dar es Salaam.


Akizungumza na Mwananchi Naibu Katibu Mkuu wa Chadema- Zanzibar, Salum Mwalimu amesema mbunge huyo alikuwa njiani kurudi nyumbani kwake Pemba visiwani Zanzibar.

Pia amesema alipaswa kuhudhuria kikao cha kamati kuu ya chama hicho kilichofanyika siku ya
Jumapili febuari 10 2019

“Ni kweli amepata ajali, japo hatujapata taarifa za kitabibu zaidi ila ameumia katika eneo la kifua na alipatiwa huduma ya kwanza katika Hospitali ya Dumila baadaye akapelekwa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Morogoro na sasa wapo katika utaratibu ili wawalete Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH),” amesema Mwalimu.

hata hivyo abiria wengine waliokuwamo katika gari hiyo pamoja na dereva wamepatiwa huduma ya kwanza na watapelekwa Muhimbili kwa uchunguzi zaidi.