Mbunge wa jimbo la Welezo Sada Mkuya Salum amekabidhi kadi za bima ya wafya kwa wzee 105 wa jimbo lake jana.

IMG_20160719_113254 (1)

Mbunge Sada Mkuya na Mkuu wa Wilaya ya Magharibi A Mwinyiussi Abdallah Hassan wakikabidhi kadi hizo

IMG_20160719_113307

Jumuiya ya wastaafu na ya wazee Zanzibar  wamesema  mbali na kuahidia kusaidiwa matatizo mbalimbali ikiwemo ya kijamii ikiwemo kuanzishiwa  utaratibu wa pesheni jamii  lakini bado wanakabiliwa na matatizo mbalimbali ikiwemo  kusumbuliwa na magonjwa yasiyoambukizwa.

Akisoma risala ya wazee katika ghafla ya kukabidhiwa kadi ya bima za afya kwa wazee wa jimbo la Sebleni  Betha Methya Lukanguzi amesema  kwa kipindi kirefu wamekuwa wakisumbuka katika kupatiwa matibabu kutokana na kukosa  kipato cha kulipia hospitalini.

Akikabidhi bima za afya kwa wazee hao Mbunge wa jimbo la Welezo Sada Mkuya amewaomba  wafanyakazi wa hospitali za serikali na bianafsi kutowa huduma  bora na kwa wakati kwa wazee hao ili waweze kuondokana na matatizo wanayokumbana nayo wanapohitaji kutibiwa ikiwemo kucheleweshewa matibabu na kutolewa maneno ya kashfa.

Akizungumzia suala la baadhi ya watu kusema huduma ya matibabu haiwafikii walengwa alifahamisha kuwa kila mzee wa miaka 65 ndiye ataenufaika na huduma hiyo na wazee kuazia miaka 40 ambao hawawezi kujikimu kimatibabu.

Akizinduwa ugawaji wa kadi hizo kwa wazee hao mkuu wa wilaya ya magharibi A Mwinyi Ussi Abdallah amesema kila kiongozi anajukumu la kuunga mkono juhudi za serikali katika kuwasaidia wananchi wa majimboni mwao na kuondokana na tofauti za siasa zinazorejesha nyuma shughuli za maendeleo Nchini.

Jumla ya wazee 105 wamepatiwa bima ya afya katika shehia mbili za jimbo hilo kwa lengo la kupatiwa matibabu ya uhakika wanapokwenda hospitalini.