Mbunge wa Rombo (Chadema), Joseph Selasini amejiuzulu wadhifa wa Mnadhimu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kutokana na kutotambulishwa rasmi kwa uongozi wa Bunge tangu ateuliwa miaka miwili iliyopita.

Selasini aliteuliwa kukaimu wadhifa huo miaka miwili iliyopita, kufuatia aliyekuwa akishikilia wadhifa huo, Tundu Lissu kuwa katika matibabu nje ya nchi baada ya kushambuliwa kwa risasi zaidi ya 30 na watu wasiojulikana Septemba 7, 2017 nyumbani kwake Jijini Dodoma.