Mbunge wa Ukerewe Joseph Michael Mkundi ametangaza kujiuzulu uanachama na nyadhifa zake zote ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema na kuomba kujiunga CCM.

Jana Oktoba 10 Mkundi amemtumia barua Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Tanzania Mhe. Job Ndugai akimueleza dhamira yake ya kujivua Uanachama Chadema na kujiuzulu nafasi yake ya Udiwani katika Kata ya Bakiko na Ubunge katika jimbo la Ukerewe.

Amesema amechukua uamuzi huo kutokana na kukosa ushirikiano kutoka kwa viongozi wenzake wa Chadema wakati wa ajali ya MV Nyerere iliyotokea Septemba 20 mwaka huu.

Soma taarifa yake hapo chini: