Mchezo wa mpira wa meza Tanzania kuboroshwa kimataifa

Chama cha mpira wa meza Zanzibar kwa  kushirikiana chama cha mpira wa Meza Tanzania  Bara kwa pamoja vimejipanga kuhakikisha mchezo huo unakuwa na wachezaji wengi wa kushindana mashindano ya kimataifa.

Akizugumza na Zanzibar24 Msemaji wa chama cha mchezo wa mpira wa meza Zanzibar Abubakar Khatibu kisandu pia ni mjumbe wa chama hicho amesema moja ya mipango yao wamendaa semina kushirikiana na kamati ya Onlimpiki Tanzania kwa lengo la kuboresha mafunzo ya mchezo huo.

Aidha kisandu amesema mafunzo yameshirikisha  wakufunzi saba kutoka Zanzibar na Tanzania bara yanayondaliwa na kamati ya Onlimpiki ,kwa upande wao chama cha mpira wa meza Zanzibar  (ZTTA) wameteua walimu wa somo la elimu ya michezo ili kuwapa ujuzi wa kuelewa mchezo huo kwa kuwa ndio mabalozi wazuri kwa wanafunzi.

Kwa upande mwengine kisandu amempongeza Raisi wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein kupitia wizara ya Vijana,Sanaa na michezo  kwa hatua yake nzuri ya kuwatengea kiwanja maalum katika uwanja mpya wa Mao Tsung.

’ni jambo la faraja sana kupitia wizara ya vijana sanaa na michezo kutujengea ukumbi maalum la mpira wa meza ni jambo kubwa sana tena sana sasa wachezaji wengi watajitokeza kuucheza mchezo huu’’ Alisema kisandu.

Kisandu amesema mchezo huo umekumbwa na changamoto ya Viwanja kwa muda mrefu sana baada ya kutumia

mikumbi ya maskulini ambayo imekuwa na changamoto kubwa ya matumizi ya skulini.