MSHAMBULIAJI wa timu ya Simba, Meddie Kagere ‘MK14’ amechaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa mwezi Februari wa Ligi Kuu Tanzania Bara (TPL) msimu wa 2018/2019.
Kagere raia wa Rwanda ametwaa tuzo hiyo baada ya kuwashinda wenzake wawili, Salim Aiyee wa Mwadui na Salum Kimenya wa Prisons alioingia nao fainali katika uchambuzi uliofanywa Dar es Salaam wiki hii na Kamati ya Tuzo ya TPL inayotolewa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF). 

Kagere ambaye hivi sasa yupo Algeria ambapo timu yake ya Simba itacheza na JS Souira katika mchezo wa klabu bingwa Afrika amewashukuru mashabiki wake kupitia akaunti yake ya instagram.