Meneja awaadhibu wafanyakazi kwa kuwanywesha Mkojo na Mende

Kwa mujibu wa Gazeti la Morning Post limearifu kuwa Mameneja watatu wa Kampuni moja ya Kichina wamefungwa jela kati ya miaka mitano na kumi kutokana na tukio la kuwaadhibu wafanyakazi walioshindwa kufikia malengo ya mauzo ya kibiashara kunywa mkojo na pia kula mende.

Polisi Nchini humo wamechukua hatua baada ya video kuowaonesha wafanyakazi hao wakichapwa kwa mkanda na kunywa kitu chenye rangi ya njano ambacho kinadaiwa kuwa ni mkojo.

Video hiyo imekuwa maarufu mitandaoni na watu kutumiana kwa wingi kwenye mitandao nchini China na tovuti mbali mbali ikiwemo tovuti ya Weibo iliyoweka video inayomuonesha muajiri wa kiume akiwa amesimama katikati ya mduara akipigwa mjeledi.

Taarifa za hivi karibuni zinaarifu kuwa kumekuwa na mifano ya kesi kama hizo kwa wafanyakazi kupigana makofi wenyewe kwa wenyewe kwa lengo la kuongeza ari kazini, na wafanyakazi kulazimishwa kutambaa barabarani ama kubusu mapipa ya takataka kama adhabu au kuongeza mshikamano kazi.

Kampuni hiyo pia inaarifiwa kushindwa kuwalipa wafanyakazi wake mishahara kwa muda wa miezi miwili iliyopita, na wafanyakazi walikuwa na hofu ya kuzungumzia suala hilo kwa kuhofia kupoteza malipo yao endapo pia wataacha kazi.