Meneja wa msanii Diamond Platnumz, Sallam SK amethibitisha kukutwa na virusi vya ugonjwa wa Corona.

Sallam ameyasema hayo kupiti akaunti yake ya kijamii ya Instagram, ambapo amesema kuwa majibu ya vipimo alivyopima ameonekana akiwa na virusi vya Corona.

”HABARI…!! Napenda kuwajulisha na kuwatoa hofu ndugu, jamaa na marafiki kuwa nimepata majibu ya vipimo na nimeonekana nikiwa na Corona Virus.” Ameandika Sallam SK kupitia Instagram.

Hata hivyo meneja huyo wa msanii mkubwa barani Afrika ameongeza kuwa ”Kwa sasa nipo chini ya uwangalizi mzuri na afya yangu inaendelea vizuri, pia niishukuru serikali kwa maandalizi mazuri na huduma nayopata wodini, Kwenye kituo toka juzi nipo peke yangu kama nimekikodisha vile, wahudumu wanaushirikiano mzuri Mungu awalinde na awape afya njema maana wamejitolea nafasi zao kutupatia huduma sisi waathirika, hili janga la kimataifa linakwepeka kama tutafuata ushauri nasaha kutoka kwenye Wizara husika, naomba kwa wote tuwe salama na familia zetu, tuchukue tahadhari mapema. Be Strong and Be Safe Everyone out there.”