Mfanyabiashara maarufu Tanzania Mo Dewji ametekwa na watu wasiojulikana

Mfanyabishara maarufu nchini ambaye pia ni muwekezaji wa klabu ya Simba, Mohammed Dewji (MO) amedaiwa kutekwa na watu wasiojulikana, saa 11 Alfajiri ya leo Oktoba 11.

Imeelezwa Mohammed ametekwa na watu walio na silaha za moto wakati akiingia Gym ya Collesium iliyopo Oysterbay jijini Dar es Salaam alipokuwa akiingia kufanya mazoezi..

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Lazaro Mambosasa amesema kwamba wameweka vizuizi kuhakikisha hakuna mtu anayetoka, ili watekaji wasitoke nje ya nchi, na kwamba waliohusika kwenye tukio la kumteka Mo Dewij ni raia wawili wa kigeni (wazungu).

Mambosasa amesema kuwa tayari wameweka vizuizi kuhakikisha hakuna anayetoka, ili watekaji wasitoke nje ya nchi.