Imeelezwa kwamba mfumko wa bei umeshuka  hadi kufikia asilimia 0.7 kwa mwezi wa Machi 2020 ukilinganisha na asilimia 0.8 katika mwezi February 2020.

Hayo ameyasema Mkuu wa Takwimu wa Serikali  wa mfumko wa bei Khamis Abdul-rahmani Msham huko katika Ofisi za Mtakwimu Mkuu Wa Serikali Mazizini wakati akiwasilisha  takwimu za bei kwa vyombo vya habari .

Amesema miongoni mwa bidhaa zilizoshuka ni pamoja na vyakula ikiwemo mchele   na ndizi mbichi, vinywaji visivyo kilevi,  pamoja  na mafuta ya taa, Petrol na Diesel.

Nae Afisa uchumi wa Masoko ZURA Omar Ali Yussuf  ameeleza kuwa  bei za mafuta zinatarajiwa kushuka zaidi kutokana na hali iliyopo .

Aidha amefahamisha kuwa mafuta ya ndege yameshuka kwa kipindi hiki na uzalishaji wake umekuwa mkubwa katika soko la dunia kutokana na hali iliopo ya ugonjwa corona na kusitishwa kwa safari  hivyo  usafiri wa  ndege umepungua.

 Kwa upande wake Dkt Deogratius Philip Macha msaidizi Idara ya Uchumi kutoka Benki ya Tanzania BOT amewataka wananchi kuondoa hofu na wasiwasi wa upungufu wa chakula kwani chakula kipo cha kutosha . 

Na Mwashungi Tahir:Maelezo Zanzibar.