Mkutano Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa utafanyika jijini Dodoma leo ambapo kikubwa ni kupiga kura ya kumpitisha mgombea wa Urais wa Tanzania na kuwasilisha taarifa za Serikali za Tanzania na Zanzibar zoezi litakalofanywa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi.