Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharib Ayoub Muhammed Mahmoud amewataka wananchi wa Mkoa huo kuwa tayari kuchangia damu ili kuweza kuokoa vifo kwa wagonjwaa wanaohitaji huduma ya damu kwa matibabu.

Akizungumza na Waandishi wa Habari  ofisini kwake Vuga Mjini zanzibar kuhusiana na ghafla hiyo inayotarajiwa kufanyika  tarehe 4 mwezi wa tano mwaka huu katika viwanja vya maisara Mjijini Unguja.


Amesema katika kipindi cha mfungo huo wa ramadhani si vyema watu kuchangia damu kutokana na hali ya kiafya ambapo katika kipindi hicho cha mwezi mzima kumekuwa  na mahitaji makubwa kwa kitengo cha damu salama ambapo kinahitaji ujazo wa unit
1700.

Katika hatua nyengine Mkuu wa Mkoa amesema kitengo hicho cha damu salama kimesha kusanya unit 1400 katika kipindi hichi kwa ajili ya matumizi ya  mfungo wa ramadhani na kwamba wameshatumia unit 400 kwa muda wa wiki mbili zilizopita hivyo bado kunahitajika kuchangia damu iki kufikia malengo hayo.

Mkuu huyo wa Mkoa amesema kutokana na kutumika kwa ujazo wa unit 400 bado inahitajika ujazo wa unit 800 hivyi Mkoa wa Mjini Magharibi inatarajia kuchangia zaidi ya unit 1000 ili kuounguza tatizo hilo.

Mgeni rasmi wa hafla hiyo anatarajiwa kuwa
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi.


Na:Fat-hiya Shehe Zanzibar24