Kaimu Mkuu wa mkoa wa kusini unguja  mhe; Idrissa Kitwana Mustafa amesema Serikali mkoani humo itaendelea kusimamia vyema amri iliyotolewa na Rais wa zanzibar Dkt. Ali Moh’d Shein ya kuzuia kuendelea kwa ujenzi  wa eneo la binguni uwanja wa ndege lililokusudiwa kujengwa hospital ya rufaa ya mkoa huo.

Mhe, Kitwana ametoa kauli hiyo katika eneo hilo la binguni wakati alipofanya ziara ya kulikagua eneo hilo akiwa na viongozi na watendaji mbali mbali wa Serikali pamoja na kamati ya ulinzi na usalama wa mkoa huo.

Amesema amri hiyo itaendelea kuheshimiwa na kubaki kama ilivyo hadi pale Serikali kuu itakakapojiridhisha na kutoa maamuzi yake ya mwisho.

Aidha kaimu huyo amemtaka sheha wa shehia hiyo ya binguni kulikagua mara kwa mara eneo hilo ili kuona kwamba eneo hilo linabaki kama lilivyo.

Nae mkuu wa wilaya ya kati ndugu mashavu saidi sukwa ameutaka uongozi wa wizara ya afya kufuatilia kwa karibu maendeleo ya eneo hilo ili kuona kwamba Serikali inatimiza azma yake ya kufanikisha kwa ujenzi wa hospital ya rufaa kama ilivyokusudiwa.

Mnamo mwezi wa August mwaka huu Rais wa zanzibar na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi Dkt. Ali Moh’d Shein ameshtushwa na baada ya kuona eneo lililotengwa kwa ajili ya kujengwa hospital ya rufaa na kuuziwa afrika muslim agency kujenga kijiji cha watoto yatima, kituo cha afya na skuli.

Na: Rauhia Mussa.