Mhe. Ayoub amtumbua sheha wa Chuini Unguja

Kufuatia malalamiko ya wananchi wa shehiya ya Chuini wilaya ya Magharib A Unguja Kunyang’anywa Hekari zao na kukwatwa viwanja kwaajili ya ujenzi wa makaazi ya watu wengine, Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharib Unguja Mhe. Ayoub Mohammed, Jana Oktoba 11 ametengua uteuzi na kumfuta kazi Sheha wa Shihiya ya Chuini Bw Juma Moh’d Khatib kwa kosa la kujihusisha na migogoro ya ardhi katika shehiya hiyo.

Akizungumza katika ziara aliyoifanya katika shehiya hiyo Mhe. Ayoub amesema migogoro ya ardhi haiwafurahishi wakaazi wa eneo hilo kutokana na kunyang’anywa ardhi zao.

Hivyo amewataka viongozi wa mkoa huo kutojihusisha na migogoro ya ardhi na badala yake kuisaidia Serikali katika usimamizi na kuishauri vyema kuyaendeleza maeneo ya kilimo kwenye shehiya na wilaya zao.