Msanii mkongwe wa Hip Hop hapa Tanzania, Sugu ametangaza rasmi kustaafu muziki, kwa maelezo kuwa kwasasa atajikita kwenye majukumu mengine.

Sugu amesema kuwa anaamini ameutoa mbali muziki wa Hip Hop Tanzania, hivyo kwa sasa anajiandaa kuangalia namna ya kustaafu kwa kuwaachia mashabiki wake zawadi ya mwisho.

Nimefanya MUZIKI kwa miaka mingi sana sasa, nakiri umenitoa mbali sana nami nimeutoa mbali mpaka hapa ulipofika na mchango wangu kwenye GAME la Bongo na African Hip-hop si haba …Lakini kuliko kuwa kimya bila kuwa ‘active’ kimuziki nadhani sasa nalazimika kufikia mwisho na soon nitaweka rasmi MIC chini. Umri nao unasonga na MAJUKUMU mengine yanayohitaji muda wangu zaidi yanaendelea kuongezeka kwa neema zake MUNGU,“ameeleza Sugu kupitia ukurasa wake wa Instagram na kuwaahidi mashabiki wake jambo “Suala ni FANBASE yangu naiagaje wakati utakapofika? Kwa ALBUM au just a CONCERT,“.

Joseph Mbilinyi maarufu kama Sugu ni moja ya wasanii wakongwe wa muziki wa Hip Hop ambao wameanza muziki miaka ya 1990’s.