SMZ kuja na mpango wa ujenzi wa nyumba za kisasa Unguja na Pemba

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imesema katika kuhakikisha miji ya Zanzibar inapendeza na kuwa na hadhi ya kisasa imeanzisha mpango maalum wa uendeshaji wa miji ikiwemo ujenzi wa nyumba za kisasa katika miji iliyopangwa vizuri.

Akijibu swali la Mwakilishi wa Jimbo la Mtambile Naibu Waziri wa Ardha,Nyumba,Maji na Nishati Juma Makungu Juma amesema katika kupanga miji serikali imetayarisha mipango ya kuendeleza miji katika visiwa vya Unguja na Pemba.

Amesema mkakati wa taifa wa maendeleo ya Ardhi unaelekeza Zanzibar iwe na miji mikubwa miwili mmoja Unguja na mwengine Pemba ambao ni Chakechake.

Aidha mkakati huo unaendeleza upangaji wa miji midogo 14 kati ya hiyo mitano iko Pemba ambayo ni  Mkoani, Wete, Micheweni, Kengeja na Konde  kwa kupitia mradi wa huduma za jamii mjini ZUSP.

Amani Omar.