Mkandarasi aliyefahamika kwa jina la Boniface Exavery, ambaye alitengeneza madirisha ya Almunium na katika Kituo cha Afya cha Katumba, Halmashauri ya Nsimbo ya mkoani Katavi, ameyavunja madirisha hayo, kwa kile alichokidai kutokamilishiwa malipo yake na ofisi ya Halmashauri huku akiwaameshamaliza kazi.

Akizungumza mara baada ya kutembelea eneo hilo, Mkuu wa Mkoa wa Katavi Juma Homera, amedai mradi huo ulikuwa umekiuka taratibu mbalimbali za kisheria, ikiwemo upatikanaji wa tenda hiyo.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, mwenyewe ameeleza kushtushwa na hatua ya Mkandarasi huyo, na kueleza taarifa za awali walizipata kutoka kwa wananchi, na kulitaka Jeshi la Polisi kumshikilia Mkandarasi huyo, huku akikiri Halmashauri kutomlipa malipo yake.