Baraza la Manispaa Mjini Unguja, limewataka wafanya biashara wote kudumisha usafi katika maeneo ya Biahara zao hilikuepukana na maradha mbalimbali yanayo weza kusababishwa na uchafu.

Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Baraza la Manispaa Mjini  Said Juma  Ahmada wakati alipo fanya ziara ya kushitukiza katika  Soko la Kuku la Darajani.Mkurugenzi huyo amewataka wafanya biashara hao kudumisha usafi katika maeneo ya Soko hilo kwakua  usafi ndio kivutio kikubwa kwa wateja wanao fata huduma katika eneo hilo.

 Aidha Mkurugenzi huyo aliwasisitiza wafanya biashara hao kuondoa vitu visivostahiki katika mazingira yao ya biashara kama kueka nguo ovyo na mikoba isiyo na kazi maalum kwani Soko limejengwa la kisasa hakuna haja ya kulichafua linahitaji kutunzwa na kuwa safi siku zote.

Kwaupande wao  wafanya biashara katika Soko hilo la kuku Ahmed Khamis na Bakari mohammed wameliomba baraza la manispaa kupitia uongozi wa soko  watengewe sehemu maalumu kwa ajili ya kuhifadhia nguo zao kipindi wanapo fika katika eneo la Biashara.

Baraza la Manispaa Mjini linaendelea na Ziara ya kukagua wafanya Biashara katika maeneo yote ya wilaya ya mjini Hususani katika maeneo ya Masoko.