Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya uchaguzi Dkt.Charles Mahera amevikumbusha vyama vya siasa, wagombea na wananchi kujihadhari na vitendo vitakavyopelekea uvunjifu wa amani pamoja na matamshi mabaya katika kipindi hiki cha kampeni na kusisitiza kuwa uchaguzi utakuwa huru na haki.

Dkt Mahera ameyasema hayo katika mkutano wake na wadau wa uchaguzi Mkoa wa Arusha kuwa tume imejipanga kusimamia uchaguzi kwa kufuata katiba ya nchi ya mwaka 1977, sheria za uchaguzi,kanuni na miongozo mbalimbali.

Aidha Amefafanua kuwa katika uboreshaji wa daftari la kudumu la mpiga kura Tume ilitumia billioni 157 na katika zoezi la uchaguzi inatarajia kutumia Bilioni 331 ambapo tayari wamesapokea zaidi ya bilioni 20 na maandalizi yametimia kwa zaidi ya asilimia 80.

Dkt Mahera alisema kuwa Kati ya wapiga kura 29,188,347 walioandikishwa wanawake ni 14,496,604 ambao ni sawa na 49.67%,vijana wenye umri wa Miaka 18-35 ni 15,650,998Vijana wa kiume Ni 7,804,845 na wa kike Ni 7,846,153 Aidha kuna jumla ya watu wenye ulemavu 13,211na Kati yao 2,223 Wana ulemavu wa macho ,4,911 Wana ulemavu wa mikono,6,077 Wana ulemavu wa aina nyingine

Aidha aliwataka wadau hao kwenda kutoa Elimu kwa jamii na kuwaasa kwenda kumsikiliza Sera ili waweze kumchagua kiongozi wanaompenda Akichangia Mara katika kikao Askofu wa Kanisa la Menonite Amos Mhagachi alisema kuwa Ni vyema take makundi yanayifanya fujo katika kipindi Cha Kampeni wachukuliwe hatua za kisheria ili Amani iliyopo uendelee kutunzwa.