Mkurugenzi wa Ufundi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Zanzibar Salum Ali Haji (Kocha Salu) amejiuzulu wadhifa wake huo kuanzia Jana Tarehe 13 Februari 2020.

Akitangaza uamuzi wa kujiuzulu kwa Kocha Salu, Msemaji wa ZFF Adam Natepe alieleza kwa waandishi wa habari kwamba Kocha Salu amechukua Uamuzi huo ili apate kushughulikia masuala yake binafsi.

Natepe pia alimtangaza Vuai Ali Shein kuwa ndiye atakuwa Mkurugenzi Mpya wa Ufundi wa ZFF.