Mkuu wa Jeshi la Niger, Jenerali Ahmed Mohamed amefukuzwa kazi zikiwa zimepita siku tano tangu Wanamgambo wa Kijihadi kuwaua wanajeshi 89 walipovamia Kambi ya Jeshi, ikiwa ni idadi kubwa zaidi ya wanajeshi kuuawa kwa siku moja

Mbali na Jenerali Mohamed, Viongozi wengine Waandamizi 3 wa Jeshi hilo wamevulia nyadhifa zao baada ya Kikao cha Baraza la Mawaziri

Kwa kipindi cha miaka 2 ambacho Jenerali Mohamed ameongoza Jeshi, kumekuwapo na ongezeko la mashambulio yanayotekelezwa na Kundi lenye Mfungamano na Al-Qaeda na Kundi la Dola ya Kiislamu (IS)

Nafasi yake imechukuliwa na Meja Jenerali Salifou Modi, huku Taifa hilo likitangaza siku tatu za maombolezo kutokana na vifo hivyo