Tume ya Haki za Binadamu(THBUB) yalaani kauli ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ya kuwaagiza Polisi kuwagonga na kuwapiga wahalifu wowote wakiwamo majambazi pindi wanapowakamata.

Tume yamtumia Makonda barua ya kumtaka afike makao makuu ya Tume Agosti 30 ili kujadili kile ilichokiona kuwa ni kejeli kwao pamoja na Jumuiya yote ya watetezi wa Haki za Binadamu.