Mkuu wa Soko Arusha akamatwa

Bw. John Ruzga ambaeye ni Mkuu wa soko kuu katika Halmashauri ya Jiji la Arusha, amekamatwa kufuatia agizo lililotolewa na mkurugenzi wa jiji hilo Dk. Maulid Madeni baada ya kubainika kuwahadaa wafanyabiashara katika soko hilo.

Anadaiwa kupokea fedha za wafanyabiashara kwa kigezo cha kwenda kuwalipia ushuru na kutozifikisha halmashauri kitendo ambacho mkurugenzi ameeleza ni kinyume cha utaratibu wa serikali na mtumishi wa umma.

Kwaupande wake Afisa Utumishi na Utawala wa Halmashauri ya Jiji la Arusha Baltazar Ngowi, amewataka wafanyabiashara katika soko hilo kudai risiti pindi wanapolipa ushuru wa vibanda.

Mkurugenzi Dk. Madeni yupo katika muendelezo wa operesheni maalum ya ukusanyaji wa mapato ikiwa na lengo la kuongeza mapato ya serikali na kudhibiti matumizi mabaya ya fedha za serikali.