Mkuu wa Wilaya Kaskazini ‘B’ alizwa na maovu yanayotendeka Kiwengwa

Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini B Unguja Rajab Ali Rajab amesema  kutokana na kukithiri  kwa vitendo vya uhalifu ikiwemo ubakaji na uuzwaji wa dawa za kulevya kwenye wilaya yake Serikali ya Wilaya haita vumilia matukio hayo itachukua hatua za kisheria ili kukomesha matendo hayo.

Akizungumza na Mwandishi wetu  Wilayani kwake amesema  kwenye wilaya ya kaskazini B kunatajika kwa uovu hasa kijiji cha Kiwengwa hivyo kupitia mamlaka aliyonayo atafanya msako kabambe  na kuwa chukulia hatua za kisheria watuhumiwa wa matukio hayo.

Rajab amesema mbali na matukio hayo lakini pia Kiwengwa kunasifika kuwepo kwa madanguro ya wanawake  kujiuza miili yao Miziki iso mipaka, ukabaji, ubakaji pamoja na watoto walio chini ya umri wa miaka 18 kushiriki kwenye vilabu vya pombe.

Hivyo ameahidi bila ya kumuhofia  mtu yeyote  atashirikiana  na Jeshi la Polisi  kuhakikisha hata yafumbia macho  matukio hayo yote ili kuiweka wilaya yake katika hali ya usalama na amani.

Amesema wananchi wa kaskazini B wamekuwa na hofu kubwa juu ya usalama wao  kwani matukio hayo zaidi hufanywa na watu ambao sio wakaazi wa maeneo hayo.

Aidha DC huyo amesema kijiji cha kiwengwa kinasifika kwa harakati za utalii ndani na nje ya nchi sasa kuwepo kwa matukio ya kihalifu ni kukitia doa  kijiji hicho,huku ukiangalia utalii ndio tegemeo kubwa la serikali katika kukuza pato la taifa na wakaazi husika.

Amesema hakuna mgeni hata mmoja ataependelea  kuingia kwenye nchi yenye matukio ya kihalifu hivyo ulinzi wa hali ya juu utawekwa kwenye maeneo ya utalii na makaazi ya wananchi ili kuwanyima fursa wahalifu.