WATU  wanane wameuawa Somalia na makumi ya wengine kujeruhiwa baada ya kutokea mlipuko wa bomu katika soko la kuuza na kununua mifugo kusini magharibi mwa nchi hiyo ya Pembe ya Afrika.

Maafisa usalama nchini Somalia wanasema kuwa, wahanga wote wa shambulio hilo la bomu ni raia waliokwenda katika gulio hilo lililoko katika mji wa Bay kwa ajili ya kuuza na kununua mifugo.