Muda mchache baada ya Klabu ya Simba kupoteza mchezo wa fainali ya Kombe la Mapinduzi, jana usiku, Mohamed Dewji ametangaza kujiuzulu kwake katika Mtandao wa Twitter

Huku akiwa ameweka na Kaulimbiu ya Simba isemayo ‘Simba Nguvu Moja’ amesema atabaki kama Mwekezaji, akiendeleza miundombinu na Soka la Vijana wa Simba

Ameandika, “Ni huruma Simba haikuwezi kushinda. Baada ya kulipa mishahara ya karibu Bilioni 4 kwa mwaka. Ninajiuzulu kama Mwenyekiti wa Bodi na nitabaki kama Mwekezaji. Simba Nguvu moja. Nitazingatia kukuza miundombinu na taaluma ya vijana!”

Klabu ya Simba ilifungwa goli 1-0 na Klabu ya Mtibwa Sugar kwenye mchezo wa Fainali wa Michuano ya Mapinduzi iliyochezwa Kisiwani Zanzibar