Moto wateketeza nyumba kiboje

Kijana mmoja amewahiswa Hospitali ya Mnazi Mmoja baada yakuathiriwa na Mtoto ulio teketeza nyumba ya Bi Fatma Damiani Mkunga (60)Mruguru Muembe shauri Kiboje.

Akithibitshwa kutokea kwa moto huo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Unguja Kamishna Msaidizi Muandamizi Suleiman Hassan Suleiman amesema kuwa mnamo tarehe 12-12-2018 majira Ya saa 2:00 Asubuhi huko Kiboje limeripotiwa kutokea tukio la moto la Nyumba Ya Bi Fatma Damian Mkunga imeteketea na moto na kushindwa kutambulika thamani Ya vitu vilivyouguwa hadi sasa.

Kamanda Suleiman ameeleza chanzo cha moto huo kuliwekwa polo la mkaa nyumbani kwake na Mjukuu wake ambalo limepata moto na hatimae kuteketeza nyumba .


Ameongeza kusema kuwa Mzimaji wa moto mmoja ambae ametambulika kwa jina la Mbarouk Hemed Khamis (30) Mkaazi Muembe shauri Kiboje amepata tatizo la moshi na kupelekea kuwahishwa hospital kwa ajili Ya matibabu .

Kamanda Suleiman ametoa wito kwa jamii kuwa waangalifu katika sehemu zao za kazi na kuhakikishaa unakuwepo usalama wao wa kutosha katika sehemu zao ambao hauwezi kuleta athari.

Rauhiya Mussa Shaaban