Mourinho afutwa kazi Manchester United


Manchester Unite yamfuta kazi Kocha Jose Mourinho ikiwa ni siku moja tu imepita tangu afungwe mabao 3-1 na Liverpool.

Aliekua Kocha wa Manchester Unite Jose Mourinho

Man United kupitia taarifa yake imeeleza kuwa imefikia uamuzi huo ili kunusuru mwenendo wa klabu katika michuano mbalimbali inayoshiriki ikiwemo EPL na klabu bingwa Ulaya.

“Klabu inamshukuru Jose kwa kazi yake nzuri wakati akiwa na Manchester United na tunamtakia mafanikio katika kazi yake hapo baadaye”, imeeleza taarifa ya klabu.

Kiungo wa zamani wa timu hiyo Michael Carrick ametangazwa kuchukua nafasi ya Jose Mourinho kama kocha wa muda wa Manchester United mpaka mwisho wa msimu huu wa 2018/19.