Mrema mbele ya Rais Magufuli kwenye Mkutano Mkuu CCM Dodoma amenukuliwa akisema “May 04, 2019 sisi TLP tulikaa tukajadili nani atuongoze, Halmashauri Kuu TLP ikasema hatuna mbadala wa JPM tukasema JPM anatosha, tukakutana tena May 08,2020 kura zote zikamuangukia JPM”.

“Baada ya May 08,2020 Halmashauri Kuu TLP kusema JPM anatosha kuwa mgombea wetu, May 09,2020 tukamuita Polepole aje, tukamualika na Msajili aje ashuhudie kuwa kikao cha TLP hakikuwa cha Magumashi na hapo tukapiga kura kisha wote wakasema tena wanamtaka JPM” -Mrema 

“TLP tumesema wewe JPM unatosha, tutafanya kampeni Nchi nzima kuhahakisha unachaguliwa tena, ombi langu kwenu CCM tujipange kuhakikisha kwenye Kata na Majimbo yote kuna mgombea wa TLP na CCM, tusing’ang’anie jimbo moja Watu wa CCM 30 ni matumizi mabaya ya rasilimali Watu” -Mrema