Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu ameeleza kuwa Tanzania imepokea msaada wa vifaa tiba vya kupambana na maambukizi ya virusi vya corona ambavyo vimetolewa na mfanyabiashara maarufu wa nchini China, Jack Ma

Vifaa tiba hivyo vimesafirishwa kuja Tanzania na Somalia, jana asubuhi vifaa vilisafirishwa pia kwenda Nchi nyingine 9 ikiwemo Kenya.

Katika vifaa hivyo  zimo mask, vifaa vya kupimia na nguo za kujikinga na corona.