Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa imewaita viongozi wa kitaifa wa vyama vya siasa ili wazungumzie utekelezaji wa sheria zinazosimamiwa na ofisi hiyo katika kikao kitakachofanyika tarehe 02 Oktoba 20 Jijini Dar es salaam.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Naibu Msajili wa Vyama Vya Siasa, Sisty Nyahoza kikao hicho kitaanza saa 2 asubuhi na
kwamba kitaanza mapema kwa kuwa Ijumaa ni siku ya ibada.

Chanzo: HabariLEO