Msanii Bongo Fleva akutwa ugangani live bila ya chenga

Mkali wa muziki wa singeli Dullah Makabila ameonekana akiwa katika mazingira ya  ugangani huku picha na videos zikisambaa kwenye mitandao ya kijamii zikimuonyesha akifanyiwa vitendo vinavyoashiria kuwa ni vya kishirikina.

Miezi kadhaa nyuma mkali huyo wa wa singeli aliwahi kuzungumza na kusema kuwa anaamini imani za kishirikina katika kazi za muziki wake ili kufanikiwa na aliongezea kwa kusema kuwa asilimia kubwa ya wasanii nchini wanatumia ushirikina ili wafanikiwe katika muziki.

Kutokana na picha hizo zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii mashabiki wamezidi kubaki na viulizo huku wengi wakiamini kuwa huenda akawa anafanya kiki kwaajili ya video ya ngoma yake mpya na wengine wakihisi kuwa ni kweli.