Msanii wa Bongo Movie Baki Boban amefariki ghafla asubuhi ya Machi 10, 2020 nyumbani kwake. Taarifa zilizothibitishwa na watu wake wa karibu zinasema kuwa Boban aliamka akiwa mzima ila ghafla baada ya kurudi kutoka msikitini kwenye swala ya alfajiri alianza kujisikia vibaya na ndipo mauti yalipomkuta

Baki Boban enzi za uhai wake

Baki Boban atakumbukwa sana kwenye ushiriki wake wa tamthilia yenye maudhui ya utapeli inayojulikana kama Bongo Dar es Salaam. Pia Boban alishiriki katika tamthilia ya Rebeca kama baba yake Albert (Burushi).

Mwili wa marehemu ulisaliwa katika msikiti wa maamur uliopo Upanga jijini Dar es Salaam na kuzikwa katika makaburi ya Kisutu.

Inna lillah wainna ilayh rajiuwn. Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi.