Msanii kutoka jamaica ‘Spice’ atoa sababu ya kubadili asili ya ngozi yake

Msanii maarufu nchini Jamaica, Spice ameamua kufuta picha zake zote zazamani na kueka picha mpya zikimuonesha akiwa mweupe tofauti na asili yake katika ukurasa wa Istagram.

Amesema kuwa sababu ya kufanya hivyo ni baada ya kuachana na menejimenti yake iliyokuwa ikimsimamia awali ambayo amekuwa akisumbuana nayo kuhusu kuachia Album.

Spice ameachia Kanda Mseto (Mix Tape) yake mpya leo iitwayo CAPTURED, ambayo watu wengi wameeleza kuwa huenda ndio imepelekea mrembo huyo kufanya hivyo.

Angalia hii hapa ni miongoni mwa nyimbo za Spice ambazo zilishawahi kufanya vizuri duniani kote.