Msanii Mpya kutoka Nigeria atoa video inayojulikana kwa jina la ”Wait”

Msanii wa muziki kutoka nchini Nigeria Akinola Olumuyiwa maarufu Akaycentric, ambaye ni kati ya wasanii kutoka nchini Nigeria wanaofanya vizuri kwa sasa ameachia video ya wimbo wake unaojulikana kwa jina la “Wait”.

Msanii huyu alizaliwa katika mji wa Benin City, mbali na kufanya muziki lakini pia ni mwandishi mzuri wa mashairi lakini pia ni Mjasiriamali.