Msanii mkongwe wa muziki wa BongoFleva, TID ameeleza kuwa amepigwa na kuumizwa vibaya na majambazi.

Kupitia ukurasa wake rasmi wa Instagram, akiambatanisha na picha ameeleza kuwa amepigwa na aliowaita Majambazi, TID ameandika;

“Washamba Bwana Wakiona tu Unasikika wanaamua kukupiga hivi …. It’s so Sad Jambazi anaeza kukufanyia chochote sababu yeye Jambazi na Yuko na Back Up za Kijambazi,” amesema.

Kwa sasa muimbaji huyo anafanya vizuri na wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la Unaniroga.