Msanii wa muziki wa Bongo Fleva,  Isabella (Miss Bella) ameonekana kutaka kuchukua nafasi ya Vanessa Mdee kwa Jux, kwa kupost picha yao ya pamoja huku akiandika ujumbe wenye utata ambao umepelekea watu mitandaoni kumcharukia.

Picha hiyo ambayo ilipostiwa na Isabella kwenye ukurasa wake wa instagram akiwa na Jux, aliandika ujumbe ambao ulikuwa ukihoji juu ya uwezo wa Vanessa kummudu Jux.

“Nyie team Vanessa mnikome, huyo boss wenu ana viuno vya kimakonde!?, niacheni nipone, mimi naitwa pipi ya kusini”, aliandika Isabella chini ya picha hiyo,” aliandika Isabella.