Mshike mshike wa ligi kuu ya Zanzibar hatua ya nane bora unaendelea kesho kwa kupigwa michezo miwili katika viwanja viwili kiwanja cha Amani na kiwanja cha Gombani Pemba hatua ya mzunguko wa Tatu .

Mafunzo watakutana na Opec kwenye dimba la uwanja wa Amani mafunzo wakiwa hawana alama hata moja baada ya michezo ya mzunguko yote miwili kupoteza wakati Opec wakiwa na alama moja baada ya kutoa sare dhidi ya Mwenge.

Kwa upande wa Dimbala Uwanja wa Gombani  kesho Jamuhuri watakutana na KVZ jamuhuri akiwa na alama tatu watakutana na Kvz wenye alama nne baada ya kuifunga mafunzo na kutoka sare dhidi ya Jku.

Michezo mengine itakutanisha mafahari wengine katika viunga mbali mbali Uwanja wa Amani Jku dhidi ya Mwenge , uwanja wa Gombani Zimamto dhidi ya Hardrock michezo hii itapigwa Alhamisi hii .

 Kwa sasa Mwenge ndio kinara kwenye msimamo wa ligi kuu ya zanzibar akiwa na alama nne.