Mbunge wa Jimbo la Mwembemakumbi Ussi Salum Pondeza akizungumza na waandishi wa habari katika Hoteli ya Maruhubi Beach Villa kuhusu mashindano ya soka ya Vijana ya Jimbo hilo yajulikanayo kwa jina la “Jimbo la Chumbuni Ndondo Carry Cup” ambapo mshindi wa kwanza atazawadiwa gari aina ya Keri na mshindi wa pili shilingi milioni moja ikiwa ni moja ya ahadi alizoto kwa wapiga kura wake.
Baadhi ya viongozi wa timu, waamuzi na wasimamizi wa mashindano ya Jimbo la Chumbuni Ndondo Carry Cup wakimsikiliza Mbunge wa Jimbo la Chumbuni Ussi Salum Pondeza (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika Hoteli ya Maruhubi Beach Villa.
Mbunge wa Jimbo la Chumbuni Ussi Salum Pondeza akionyesha moja ya jezi ambazo zitatumika kwenye mashindano ya vijana ya Jimbo la Chumbuni “Jimbo la Chumbuni Ndondo Carry Cup” yatakayoanza tarehe 14.7.2019 katika Uwanja wa Saateni.
Mwenyekiti wa mashindano ya Jimbo la Chumbuni Ndondo Carry Cup Shazil Foum Khamis akipokea ufunguo na namba ya gari ya mshindi wa kwanza alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika Hoteli ya Maruhubi Beach Villa iliopo mtaa wa Maruhubi.

Picha na Makame Mshenga.