Msimamo wa kampuni ya Nike kufuatia madai ya ubakaji yanayomkabili Cristiano Ronaldo

Kampuni ya vifaa vya michezo Nike ina wasiwasi mkubwa juu ya madai ya ubakaji ya Cristiano Ronaldo.

Kampuni hiyo ambayo ina mkataba na Ronaldo unachogharimu dola bilioni 1 ambayo ni sawa na (£768m), imesema itaendelea kufuatilia kwa ukaribu kesi hiyo.

Ronaldo 33, awali alikana kuhusika na madai hayo ya kumbaka Kathryn Mayorga katika hoteli ya Las Vegas mwaka 2009.

Bi.Mayorga, mwenye umri wa miaka 34 alikuwa mwalimu nchini Marekani ambaye alishawishika kujiunga na kampeni katika mtandao ya kijamii inayosema #MeToo movement (harakati zangu pia), wakili wake alieleza.

Kampeni hiyo ambayo inawahusisha wanawake kusimama na kufichua unyanyasaji wa kingono, ilimfanya Kathry kupata ujasiri.

Kampuni ya Nike katika maelezo yao ilisema ina wasiwasi na kesi inayomkabili na tutaendelea kufuatilia kwa ukaribu.

Kwa upande wao EA Sports ilisema “Tumeona maelezo ya ripoti kamili inayomkabili Ronaldo na tunafuafilia kwa ukaribu,

kwa sababu tunatarajia wanamichezo kutuwakilishi vyema kama mabalozi hivyo wanapaswa kufanya kazi yao kwa weledi na kwa manufaa ya EA”.

Klabu ya Juventus kutoka Italia iliibuka na kumtetea Ronaldo ambaye alijiunga na timu hiyo akitokea Real Madrdid kwa dolla milioni 99.2 mwezi wa saba.

Kwenye ukurasa wa tweet, juventus waliandika Cristiano Ronaldo alionyesha werevu mkubwa na kuitathimini klabu yetu jambo ambalo kila mmoja wetu alilifurahia.

Ronaldo ambye ni raia wa Ureno katika siku za mwanzo alisema tuhumu hizo sio za kweli, hii ni baada ya kuandikwa kwenye gazeti la Uingereza la Der Spiegel.

Siku ya jumatano Ronaldo alithibitisha kwenye akaunti yake ya twitter :’Ninapinga tuhuma zote zinazonikabili’.

‘Ubakaji ni kitendo kibaya ambacho siwezi kukifanya hata kidogo naamini katika ninachokisema. Natajitahidi kusafisha jina langu, nilikataa kuongea na vyombo vya habari kwa sababu vinatoa taarifa kwa manufaa yao bila kuangalia upande wa pili’.

Ninachoweza kusema sasa ni tusubiri matokeo ya utafiti ambayo yanaendelea.

Gazeti la Der Spiegel liliandika kuwa Bi. Mayorga alitoa ripoti katika kituo cha polisi cha Las Vegas muda mfupi baada ya tukio hilo.

Mwaka mmoja baadae, ripoti ilitolewa ikimhusu Ronaldo kukubali kutoa kitita cha dola milioni 375,000 ili kesi hiyo imalizike kimya kimya bila kutoa taarifa kwa umma kwa kulinda heshima yake.

Wanasheria wanafikiria kutangaza habari hizo na kuvunja makubaliano ya awali.

Bi Mayorga amesema kuwa alikutana na Ronaldo usiku kwenye ukumbi wa Rain ulipo katika hoteli ya Palms na Casino, ambapo mchezaji huyo alifanikisha kumbaka.

Mwanasheria wa mlalamikaji Stovall alisema Bi.Mayorga aliathirika sana na kitendo hicho na sasa anasumbuliwa na msongo wa mawazo.

Kituo cha Polisi cha Las Vegas kilithibitisha kufanya uchunguzi wa mwanzo mwaka 2009 ingawa hawakubaini kama Ronaldo ana tatizo lolote.

“Kipindi hicho ripoti inatoka mtuhumiwa hakuwa tayari kutoa ushirikiano wa sehemu ambayo tukio la ubakaji lilifanyika” alisema.

Mwezi wa tisa mwaka 2018 kesi ilifunguliwa tena baada ya kutolewa kwa taarifa waliyopewa wachunguzi wetu, Mwanasheria wa Ronaldo alisema watalishitaki Gazeti la Der Spiegel kwa kutoa taarifa za uongo ambazo zinaendelea kumchafua mchezaji wake.