Majaji wa Marekani wamezuia agizo la Rais Donald Trump lililotaka Mtandao wa TIKTOK wa China uzimwe Nchini Marekani kuanzia jana jumapili.

Sasa Watumiaji wa Tiktok nchini Marekani watandelea kutumia mtandao huo baada ya Majaji kuzuia agizo hilo la Trump saa chache kabla ya Jumapili yenyewe kufika.

Trump alizuia Mtandao huo wa China kwa madai kwamba ni tishio kwa taifa hilo kwani unaingilia usalama wa Taifa.