Jeshi la Polisi Mkoa wa Kusini Unguja linaendelea kufanya doria ya mahojiano kupitia vyombo vya maringi mawili vilivyopo katika barabara ambavyo vimepata ajali kwa kuwatambua wahusika wanaristi ilikuweza kupunguza staili mpya iliyozuka ya wizi wa honda na kupakiwa katika gari za carry.

Akizungumza na Zanzibar24 Tunguu Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja Kamanda Suleiman Hassan Suleiman amesema kuwa kuna tukio lilotokea April ishirini na sita majira ya  nne na nusu asubuhi eneo la jumbi skuli  na wahalifu wasiojulikana wameiba honda iliyokuegesha na kupakiwa katika gari ya carry .

Ameongeza kusema kuwa shauri hilo linaendelea na uchunguzi ilikuweza kuwabaini waliohusika na uhalifu huo wa wizi wa honda unaoshamiri katika maeneo tofauti ya mkoa huo wa kusini unguja.

Kamanda Suleiman ametoa wito kwa jamii kuwa makini pindi pale wanapoweka vyombo vyao vya maring mawili  katika sehemu zao na kuona kuwa kuna ungalifu ilikuweza kuepusha wizi wa honda uliozuka kwa stahili mpya pindi unapoegesha vyombo vyao katika eneo husika.

Wizi wa vyombo vya maringi kwa sasa kumezunguka na stahili ya kuchukuliwa chombo bila ya ufunguo na kuingizwa katika gari zilizowazi aina carry kwa baadhi ya maeneo ya mkoa wa kusini unguja .

Rauhiya mussa shaaban