Mtoto azaliwa baada ya kupandikiza tumbo la uzazi kutoka kwa mtu aliyekufa

Mtoto wa kike mwenye afya amezaliwa kutokana na kupandikiza tumbo la uzazi kutoka kwa mwili wa mtu aliyekufa.

Upasuaji uliofanyika kwa saa kumi, ulifanyika mjini São Paolo, Brazil, mwaka 2016.

Mama mwenye umri wa miaka 32 alizaliwa bila kuwa na tumbo la uzazi.

Kumekuwa na upandikizaji wa matumbo 39 ya uzazi kwa kutumia wachangiaji walio hai, wakiwemo wazazi wanaojitolea matumbo yao kwa mabinti zao na kufanya kuzaliwa kwa watoto 11.

lakini majaribio kumi ya upandikizaji kutoka kwa matumbo ya watu waliokufa hayakufanikiwa au wakati mwingine mimba zilitoka

Katika hatua hii mpya, aliyejitolea tumbo la uzazi ni mama wa umri wa miaka ya 40 mwenye watoto watatu ambaye alipoteza maisha baada ya kuvuja damu kwenye ubongo.

Mhitaji alikuwa na tatizo kwenye mfumo wake wa uzazi na kufanya tumbo lake kushindwa kuumbe kiumbe tumboni tatizo ambalo humkumba mwanamke mmoja kati ya kila wanawake 4,500.

Hata hivyo Ovari zake hazikuwa na matatizo.Na madaktari walikuwa tayari kuondoa mayai, kuyarutubisha kwa kutumia mbegu za kiume za mumewe kisha kuzigandisha.

Mwanamke alipatiwa dawa za kudhoofisha mfumo wake wa kinga ili kuzuia mwili wake kushambulia na kukataa mfumo wa upandikizaji mwilini mwake

‘Maendeleo yake ya kitabibu’

Katika kipindi cha wiki sita baadae, alianza kupata hedhi.

baada ya miezi saba, mayai yake yaliyorutubishwa yakapandikizwa.

Na baada ya mimba, mtoto wa kilo 2.5 alizaliwa kwa upasuaji tarehe 15 mwezi Desemba mwaka 2017.

Dokta Dani Ejzenberg kutoka Hospitali ya mjini Sao Paolo amesema upandikizaji huu wa kwanza kutoka kwa wachangiaji walio hai ulipiga hatua na kufanya kuwepo kwa uwezekano wa kusaidia wanawake wengine wengi wasio na kizazi.

”Hatahivyo, uhitaji wa kuwa na mtu wa kujitolea una changamoto kwa kuwa ni vigumu sana na mara chache sana lengo hufikiwa kwa kuwa utoaji huhitaji utayari wa familia na marafiki wa karibu”.

Dokta Srdjan Saso, kutoka chuo cha Imperial jijini London amesema majibu yalikuwa yakufurahisha sana

”Yanafanya kuwepo na ongezeko la wanaojitolea, lakini pia kunakuwa na gharama ndogo kufanikisha, hali kadhalika kupunguza hatari inayoweza kutokea kwa wachangiaji walio hai wakati wa upasuaji”.

Upandikizaji wa mfuko wa uzazi umefanywa katika mataifa 10 ikiewemo: Sweden, Saudi Arabia, Uturuki, Marakani, Uchina na Jamhuri ya Czech, Brazil, Ujerumani, Serbia na India.

  • 2014 – Mwanamke kutoka mji wa Gothenburg, nchini Sweden alijifungua mtoto wa kiume kupitia utaratibu wa kupandikizwa mfuko wa uzazi.
  • Mwanamke huyo wa miaka 36 alipata mhisani wa miaka 60 aliyempatia kizazi.
  • 2017 – Mwanamke katika mji wa Dallas, Texas, alizaa mtoto kupitia mfumo wa upandikizaji wa mfuko uzazi nchini Marekani.
  • 2018 – Mwanamke alifanikiwa kujifungua mtoto wa kisichana kupitia upandikizaji wa mfuko wa uzazi kwa mara ya kwanza nchini India.
  • Watoto 12 wamezaliwa kupitia mfumo huo nane kati ya watoto hao wamezaliwa nchini Sweden.
  • Ni mwanamke mmoja tu kati ya 12 aliyepandikizwa kizazi cha mtu aliyekufa.

Chanzo BBC. Swahili.