Kuna tetesi kuwa mtoto wa Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa ni miongoni mwa walioonyesha njia ya kugombea ubunge jimbo la Monduli kwa tiketi ya Chadema.

Leo Agosti 9, Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Arusha, Aman Golugwa amesema mgombea ubunge kwa tiketi ya Chadema jimbo hilo atajulikana Jumamosi. Amesema kuna wanachama kadhaa wa Chadema wameonyesha nia ya kugombea akiwamo  mtoto wa Lowassa, Fred Lowassa.

“Siwezi kuwataja wote kwani bado wengine hawajarejesha fomu na kuchukua ila miongoni mwa walioonyesha nia ni Fred Lowassa,” amesema.

Aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo kupitia chama hicho, Julius Kalanga alijiuzulu wiki iliyopita na kujiunga na CCM na anatarajiwa kutetea kiti hicho kupitia CCM.

Amesema baada ya kukamilika mchakato huo leo saa 10 watatoa taarifa kamili.

Amesema kikao cha kura ya maoni cha kupitisha mgombea wa Monduli kitafanyika Jumamosi.

“Kikao kitafanyika Kata ya Migungani ambako kuna uchaguzi mdogo na tunaimani tunakwenda kutetea jimbo letu,” amesema.