Mtoto Adalia Rose wa nchini Marekani anasumbuliwa na ugonjwa wa progeria ambao unamfanya mtu kuzeeka kabla ya umri wake.

Madaktari wamesema mtoto huyo anaweza akafariki akitimiza miaka 13, ambapo mpaka sasa ana miaka 12.

Kutokana na hilo, Adalia amekuwa akiishi maisha yake akiwa na furaha kwa msaada wa wazazi wake, akisema anataka kufurahi muda wake aliokuwa nao hapa duniani.