Familia ya Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Freeman Mbowe imethibitisha kuwa na mgonjwa wa Corona.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Msemaji wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), John Mrema amesema mgonjwa huyo ni mtoto wa kwanza wa Mh. Freeman Mbowe aitwaye Dudley.